Baraza la Waislamu la Fatwa Lapongeza uteuzi wa sheikh Abdulhalim Hussein Athman kama Kadhi mkuu

0

Baraza la Waislamu la Fatwa limepongeza uteuzi wa sheikh Abdulhalim Hussein Athman kama Kadhi mkuu Kenya .

Kupitia mkurugenzi wa baraza hili Sharif Ahmad Badawi na Naibu wake Sheikh Abubakar Bini ,wameelezea matumaini kuwa kadhi mkuu ataunganisha umma wa kiislamu Kenya.

“Tunapongeza jaji mkuu Martha Koome na tume ya huduma za mahakama JSC kutokana na uteuzi wao wa busara kumchangua Sheikh Abdulhalim Athman kuwa kadhi mkuu Kenya ,ana vigezo hitajika na hekima fika kutekeleza jukumu Hilo la kikatiba “Sharif Badawi

Kwa upende wake Sheikh Abubakar Bini ameelezea imani kuwa kadhi mkuu mpya ataweza kuwaunganisha waislamu wote kama walivyofanya watangulizi wake .

Sheikh Abdulhalim ni miongoni mwa watahiniwa watano wanasheria waloteuliwa kupigwa Msasa na tume ya huduma za mahakama JSC .Wadhifa huo ulivutia zaidi ya wakenya 24 waliotuma maombi yao kwa tume hiyo .

Kadhi mkuu Athman alihitimu chuo kikuu cha Azhar nchini Misri na kisha akahudumu kama mwalimu wa Madrasatul Munawar Mombasa, kisha akawa Kadhi wa Kwale, Mombasa na Isiolo ,Aidha amekuwa akishikilia wadhifa wa kinara wa kadhi mkuu kabla ya kuteuliwa kwake kuhudumu Rasmi kama kadhi mkuu Kenya .

Sheikh Athman ametambulika kwa sifa ya ukarimu, uaminifu na uwazi katika utenda kazi, masheikh wengi wamemkubali kama mwanasheria mkweli na mcha Mungu

Sheikh Athman aliyepata elimu ya Dini kutoka kwa mashekhe mbali mbali akiwemo babake Ustadh Hussein Athman Ni mkaazi wa Malindi – Kilifi county , asili yake ikiwa Kizingitini kaunti ya Lamu .

Post Author

Leave a Reply