Gavana Lusaka Apongeza Viongozi Wa Bungoma Kwa Umoja

Gavana Kenneth Lusaka amewapongeza viongozi kutoka kaunti ya bungoma kwa kuonyesha umoja wao kwenye masuala ya maendeleo.

Akiongea katika shule ya upili ya wasichana ya Chebukaka kaunti ndogo ya kabuchai kwenye hafla ya kuchangisha fedha za kusaidia katika ujenzi wa bweni la shule hiyo, Lusaka amewashukuru viongozi hao kwa umoja walionesha walipomtembelea Rais Ruto katika ikulu ya Nairobi.

Kuhusu masuala ya Elimu Lusaka amewahakikishia wazazi na walimu wakuu kwamba serikali yake imetoa shillingi Millioni Saba kwa ajili ya kulipa madeni ya karo kwa wanafunzi wanaofadhiliwa na serikali ya kaunti.

Lusaka amesema kwamba Kila mwanafunzi anayestahili kufadhiliwa kimasomo atalipiwa karo huku akitoa Wito kwa wazazi kujikwamua na kuwasaidia watoto wao badala ya kutegemea ufadhili wa serikali pekee.

Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetangula amesema kwamba kikao Chao na Rais Ruto kimezaa matunda baada ya rais Ruto kuahidi kwamba kiwanda Cha nzoia kitapokea Mtambo mpya wa kusaga miwa.

Wetangula amesema kwamba kama viongozi kutoka bungoma wamekubaliana kwa kauli moja kwamba kiwanda hicho hakitabinafusishwa Wala kuuzwa.

Gavana Lusaka aliandamana na Seneta wa Bungoma David Wakoli, Wabunge Majimbo Kalasinga (Kabuchai) John Waluke (Sirisia) Mawaziri wa kaunti na wakilishi wadi.

Leave a Reply