Maskofu Wahiza Mazungumzo Baina Ya Rais Ruto na Odinga

0

Maaskofu wa kanisa la katoliki katika eneo la kaskazini mwa bonde la ufa wamesemakuna haja ya serikali ya Kenya kwanza kufanya mazungumzo na upinzani ili kupunguza joto la kisiasa.

Wakiongozwa na Askofu Dominic Kimengich kwenye kikao kilicho kusudia kujadili mbinu au namna ya kuwaleta pamoja Rais William Ruto na kiongozi wa Azimio Raila Odinga ilikukomesha maandamano nakusuluhisha matatizo yanayowakumba wakenya.

“Kama kanisa maaskofu wote tume kutana kuangalia jinsi tutakavyofanya kama kanisa tuwezekuwaleta Rais na Raila tuone kama wanawezaongea pamoja na kuonanjia ambayo tunawezakufuata ilituweze kukomesha maandamano nakusuluhisha yale matatizo ambayo yako katika nchi yetu.”Alisema Askofu Dominickimengich.

Viongozi hao wakidini aidha wamesema endapo hatua hiyo itafaulu kutakuwa na amani nchini na hivyo basi kupiga hatua kimaendeleo.

“Kwa hiyo tayari kuna maaskofu wanafuatiliana najua wame advance sana natunatarajia kwamba jinsi kanisa imefanya itazaamatunda mema na kutuletea amani ambayo tunataka kama nchi.”alisemaAskofu.

Wamewahimiza wananchi waweze kuweka tofauti zao za kisiasa kando na kuunga mkono kuwepo kwa mazungumzo baina ya viongozi hao wawili kwa manufaa ya taifa hili.

“Kuna wale wanasema hawataki lakini tunasema tuombe ilimwenyezi mungu aweze kugusa mioyo yao walegeze mioyo iliwaweze kuona kwanza furaha ya nchi yetu.” Alisihi Dominic.

Halikadhalika, wameitaka serikali kuimarisha usalama kwa waandamanaji na vilevile mali ya wakenya ilikuzuia vifo, majeruhi na uharibifu wa mali za wakenya.

“Serikali ilipotangaza kwamba imeingilia kati yahaya mambo yote,ombi letu nikwamba serikali iwezekufanya kazi yake kwasababu kazi yakuleta usalama ni kazi yaserikali. Wako namaaskari,nawanajeshi.Mbona watu wanaendelea kuuawa?”Aliuliza Dominic.

Usalama kuwepo nchini inahitajiushirikiano baina ya wananchi na maafisa wa usalama wala sio jukumu la maafisa pekee.

Post Author

Leave a Reply