Gavana Sakaja Atoa Makataa kwa Madaktari Wanaogoma

0

Gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja, ametoa makataa ya saa 12 kwa madaktari wanaogoma kurejea kazini. Amesema serikali ya kaunti ya Nairobi iko tayari kuchukua nafasi za madaktari watakaopuuza agizo hili.

Akizungumza katika ukumbi wa City Hall, Gavana Sakaja amesema kuwa mgomo wa madaktari haukubaliki, na serikali ya kaunti tayari imewasiliana na madaktari bingwa kujaza nafasi za madaktari wanaogoma.

Gavana amesisitiza kuwa kutokuwepo kwa daktari yeyote kazini baada ya muda uliowekwa kumalizika kutazingatiwa kama kutoroka kazi.

Sakaja ametoa kauli hii baada ya kufanya mkutano na uongozi wa Chama cha Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya (KMPDU).

Na Lilian Aori

Post Author

Leave a Reply