Mgomo Wa Walimu Wa Chuo Kikuu Cha Moi Kuendelea
Maafisa wa UASU walijumuika na walimu wa Moi wakati wa maandamano katika jiji la Eldoret.
Walimu hao wametishia kuanzisha maandamano katika vyuo vikuu vyote. Wameshutumu serikali kwa kutenga vyuo vikuu.
Wamesema wamechoshwa na kuwaamuru walimu wa chuo cha Moi kutorejea shuleni kufunza hadi vilio vyao visikizwe na usimamizi wa chuo hicho. Wameshutumu serikali kwa kukubali mfuko mpya wa pesa za vyuo vikuu ila walimu wengine hawajalipwa.
Zaidi ya walimu elfu moja katika chuo hicho wamekuwa wakiandamana tangia Jumatatu kwa ajili ya kuitisha marupurupu yao ya Julai na Agosti. Maafisa wa UASU wamesema kuwa chuo hicho kimefeli kurudisha zaidi ya billion 4.2 ambayo ilitolewa kwa mpango wa pensheni ya walimu hao. Wametamka kuwa hawajatarejea kazini hadi pale malalamiko waliowasilisha yatasuluhishwa.