Mwanamme Aliye Valia Nepi Atembea Hadharani Sokoni Eldoret
Wachuuzi na Wanunuzi walisalia kubutwaa huku shuguli za kawaida zilisimama kwa muda katika soko kuu la wazi eneo la West mji Eldoret pale mwanamme mmoja alijitokeza kuzunguka soko hilo akiwa amevalia Nepi.
Mwanamme huyo aliyetambulika kama William Getumbe alisema lengo lake kuu ni kutoa hamasa ya uma ili kuondoa unyanyapaa ulioko katika jamii dhidi ya wanaume na watu wazima wanaotumia nepi.
Baadhi ya watu walimpokea wakisema ni hatua bora ya kutoa hamasa kuhusu matumizi ya Nepi miongoni mwa watu haswa wanaume wanaokabiliana na magongwa tofauti.
Wengine wao walisema hatua yake ni jambo ambalo bado halijawahi shuhudiwa humu nchini na linachukuliwa kama aibu ,wakimkosoa kwamba huenda anakasoro ya kiakili.
Hata hivyo,Getumbe ambaye anadai kuathirika na ugonjwa uliompelekea kukumbwa na tatizo la kupitisha mkojo,anasema ataendelea kutoa hamasa kuhusu tatizo hilo ili kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu wale wanaotumia Nepi.