Usalama wa vyakula ,wafanyakazi na mantari Bora wakati wa kongamano la ugatuzi

0

Kaunti ya Uasin Gishu imeweka mikakati ya kuhakikisha ya kwamba vyumba vya burudani na vile vya malazi, ubora wa vyakula, mathari na usalama wa wageni watakaokuja kushiriki kongamano la ugatuzi wa mwaka huu wa 2023 ni wa kiwango cha juu.

Kulingana na Mkurugenzi wa idara ya maswala ya kudhibiti vileo katika kaunti hiyo Koiya Arap Maiyo, kaunti ya Uasin Gishu iko tayari kupokea wageni wote kwa minajili ya hafla iyo.

Koiya anasema ya kuwa kama idara wameweza kukagua vyumba hivyo na kwamba vitatosheleza wageni . Amewarai wakaazi kuweza kupokelea wageni hao kwa njia spesheli.

Koiya aidha amewahakikishia wote kwamba ukaguzi utakuwa ukiendelea muda huo wote kuhakikisha usalama wa vinywaji,wafanyakazi na ubora wa vyumba vya malazi unadumishwa.

Post Author

Leave a Reply